AZAM FC:TUNAIHESHIMU YANGA...LAKINI KICHAPO KESHO LAZIMA

Jaffer Iddy Maganga, msemaji wa Azam Fc
WAKATI kesho inashuka katijka dimba la Taifa kuwakabili mabingwa watetezi wa michuano ya kombe la Kagame Yanga kawenye mchezo wa fainali ya michuano hiyo, timu ya soka ya Azam Fc imesema inawaheshimu wapinzani wao hao lakini kesho itawashushia kipigo kitakatifu na hatimaye kutwaa ubingwa huo.
Msemaji wa timu hiyo Jaffer Iddy ameiambia blogu hii leo kwamba wamejipanga vema kuhakikisha wanaifunga Yanga katika mchezo wao huo na hivyo kuendeleza ndoto zao za kuleta mapinduzi katika soka nchini.
Alisema kikosi cha Azam chote kipo katika hali nzuri huku wakiwa na ari kubwa ya mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa mgumu kutokana na Yanga pia kutaka kutetea ubingwa wao.
Maganga alisema wanahaki ya kujivunia kikosi hicho kutokana na ubora ilichonacho ambapo kwa uchanga wa timu hiyo wameweza kupata mafanikio kwa haraka katika siku za hivi karibuni ikiwemo kutwaa ubingwa wa Mapinduzi, kushika nafasi ya pili ya Ligi Kuu Bara na Michuano ya kombe la Urafiki.
Kama hiyo haitoshi, Azam imetoa mfungaji bora, kocha bora, timu yenye nidhamu na mchezaji bora.