AZAM FC WATHIBITISHA MICHUANO YA BANC ABC SUPER 8

MABINGWA wa kombe la Mapinduzi Azam Fc imethibitisha kushiriki michuano ya maalum ijulikanayo kama Banc ABC Supe8r Soccer Tournament inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Agosti 4 hadi 18 katika miji ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha na Zanzibar.
Michuano hiyo itakayoshirikisha timu nane kutoka Tanzania BAra na Visiwani ina lengo la kuzipa makali timu shiriki kabla ya kuanza kushiriki katika msimu mpya wa ligi.
Habari zilizoppatikana toka klabu ya Azam zinaeleza kwamba klabu hiyo imeshawasilisha barua ya uthibitisho wa kushiriki michuano hiyo katika Shirikisho la Soka tanzania (TFF).
Awali kulikuwa na taarifa za chinichini kwamba vilabu vya Simba, Azam na Yanga vilikuwa na mpango wa kutoshiriki mivhuano hiyo kutojkana na sababu tofauti ikiwemo wachezaji wake kuchoka na pia kutojua uwazi juu ya michuano hiyo