'AZAM FC HAIKUBEBWA KAGAME '

BARAZA la vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limeipongeza timu ya soka ya Azam kwa kufika fainali ya michuano ya ukanda huo maarufu kama Kagame inayotarajiwa kufikia tamati kesho kwa timu hiyo kucheza fainali dhidi ya Yanga kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa CECAFA NIcholaus Musonye ameiambia DINAISMAIL BLOGU kwamba Azam imefika hatua hiyo kutokana na ubora iliyonayo na si kwa kubebwa.
Alisema timu hiyo ambayo imeshiriki kwa mara ya kwanza michuano hiyo na kufika hatua ya fainali ilionyesha kiwango kikubwa katika michezo yake yote na hatimaye kufika fainali.
"Sisi CECAFA tunaipongeza sana Azam Fc kwa kufika hatua hii ambayo ni jitihada zao wenyewe si kama ilibebwa...ni timu ndogo lakini imeleta upinzani mkubwa kwa vigogo,",alisema.
Aidha, Musonye alizipongeza timu za Tanzania Azam na Yanga kwa kutinga hatua ya fainali ya michuano hiyo ambapo mshindi ataondoka na dola 30,000, mshindi wa pili atapata dola 2o,000 na mshindi wa tatu atapata dola 10,000.