ARON NYANDA:AMWAGA SERA ZAKE ZA KUGOMBEA YANGANyanda ambaye anagombea Ujumbe wa Kamati ya Utendaji alipata kuwa mchezaji wa Yanga katika miaka ya 2000, pia aliwahi kuzichezea timu za Abajalo, Barcelona na Toto African zote za Mwanza.Pia alikuwa waziri wa Michezo katika Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kwa vipindi viwili wakati anasoma. 
Nyanda ambaye kwa sasa ni mfanyakazi wa benki ya NMB kama Ofisa Biashara anasema ameamua kugombea Yanga ili kuifanya iwe imara, kuwafanya wanachama wajitambue, kuhakikisha timu inakuwa bora na uchumi madhubuti. 
Anasema iwapo atachaguliwa kushika nafasi hiyo kwa kushirikiana na wenzake atakahikisha Yanga inapata mapinduzi makubwa katika mambo hayo na hasa ikizingatiwa kuwa ni klabu konge katika ukanda wa Afrika MAshariki na Kati. 
“Nawaomba wanachama wa Yanga wanichague kwa maendeleo ya klabu na soka la Tanzania kwa ujumla kwani ninafahamu udhaifu wote hivyo nitaushughulikia ipasavyo,”anasema.