ALHAJ RAGE AFANYIWA UPASUAJI INDIA


Na Princess Asia
MWENYEKITI wa Simba SC, Alhaj Ismail Aden Rage, ambaye pia ni Mbunge wa Tabora (CCM), jana amefanyiwa upasuaji wa mgongo jana katika hospitali ya APOLO, India.
Daktari wa Simba SC, Cossmas Kapinga ameiambia BIN ZUBEIRY leo kwamba, sababu ya Rage kufanyiwa upasuaji huo ni maradhi yanayojulikana kitaalamu kama Lumbar Disc Prolapse.
Dk Kapinga alisema Rage, ambaye pia ni mmiliki wa kituo cha Radio cha Voice Of Tabora (VOT) yuko kwa muda wiki moja nchini India akipatiwa matibabu na baada ya upasuaji huo wa jana, anaweza kupewa ruhusa kuanzia kesho kurejea nchini.
Kabla ya kuwa Mwenyekiti wa Simba SC, Rage alikuwa kiungo wa klabu hiyo miaka ya 1970 na miaka ya 1980 aliwahi kuwa Kaimu Katibu Mkuu, wakati pia amekuwa Katibu wa Shirikisho la Soka Tanzania (enzi za FAT), Makamu wa Pili wa rais wa TFFna Mjumbe wa Kamati mbalimbali za Shirikisho la Soka Afrika (CAF)
CHANZO:http://bongostaz.blogspot.com