ABDALLAH JUMA AIBEBA SIMBA ZENJI, AZAM YATOKA SARE

MSHAMBULIAJI mpya wa mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania BAra Simba, Abdallah  Juma jana aliiwezesha timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya mafunzo kupitia michuaono ya kombe la Urafiki inayoendelea visiwani Zanzibar.
Juma aliyesajiliwa kutoka Ruvu shooting alifunga mabao hayo katika dakika ya 27 na 44 baada ya kuzitendea haki pasi nzuri za  Patrick  Mbivayanga.Huku bao la mafunzi lilipachikwa na Jaku Joma katika dakika ya 80.
Awali maabindwa wa kombe la Mapinduzi Azam FC walikipiga na timu ya Taifa ya vijana wenye umri wa miaka 21 ya zanzibar 'Karume Boys' na kutoka sare ya bao 1-1.