ZANZIBAR HEROES KUAZWADIWA VESPA

SERIKALI ya mapinduzi ya Zanzibar imeahidi kutoa zawadi ya pikipiki aina ya Vespa kwa kila mchezaji wa timu ya Taifa 'Zanzibar Heroes' iwapo kikosi hicho kitafanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya kombe la Kagame inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi mwishoni mwa mwezi huu jijini Dar es Salaam.