YANGA SC WATISHIA KUWAFUTA UANACHAMA WAKOROFI

BARAZA la wazee la klabu ya Yanga limemjia juu mwanachama mwenzao Abeid Falcon baada ya kuwawekea pingamizi wagombe wote wa uongozi katika klabu hiyo, kupitia uchaguzi utakaofanyika Julai 15.
Hatua hiyo inafuatia Falcon kuwasilisha pingamizi kwa wagombea hao , Katiba ya Yanga na Kamati ya Uchaguzi.
Akizungumza jijini leo, katibu wa baraza hilo Ibrahim Akilimali amesema kwamba Falcon anajichanganya kwani aliwahi kugombea uongozi katika uchaguzi uliopita kupitia katika hiyo aliyodai ina mapungufu.
Kwa mantiki hiyo Mzee Akilimali alisema Falcon ni mmoja ya wanachama wakorofi ambao baada ya uchaguzi inabidi wafutwe uanachama.
Aidha, Akilimali amewataja wanachama wengine wakorofi ambao wanapaswa kufutwa uanacha wakiwemo wale wa Tawi la Uhuru na wengineo (majina kapuni