Skip to main content

WAZIMBABWE KUCHEZESHA TAIFA STARS, GAMBIA


Waamuzi kutoka Zimbabwe ndiyo watakaochezesha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia hatua ya makundi Kanda ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Gambia itakayochezwa Juni 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
Kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) mwamuzi wa kati atakuwa Ruzive Ruzive. Waamuzi wasaidizi ni Salani Ncube na Edgar Rumeck wakati mwamuzi wa akiba ni Norman Matemera. 
Kamishna wa mechi hiyo itakayoanza saa 10 kamili jioni ni Fanie Wallace Mabuza kutoka Swaziland wakati mtathmini wa waamuzi (referee assessor) ni Ali Baligeya Waiswa. 
Waamuzi hao watawasili nchini kesho (Juni 8 mwaka huu) saa 1.20 usiku kwa ndege ya Kenya Airways wakati Kamishna wa mechi hiyo atawasili siku hiyo hiyo saa 12.50 jioni kwa ndege ya South African Airways. Mtathmini wa waamuzi atatua pia Juni 8 mwaka huu saa 7.55 mchana kwa ndege ya Kenya Airways. 
Taifa Stars inayodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager inaendelea na mazoezi leo saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam chini ya Kocha Mkuu Kim Poulsen.

GAMBIA KUWASILI LEO USIKU
Timu ya Taifa ya Gambia (The Scorpions) ambayo awali ilikuwa iwasili nchini leo (Juni 7 mwaka huu) saa 1.40 asubuhi sasa itawasili leo saa 9.20 usiku kwa ndege ya Kenya Airways tayari kwa ajili ya mechi dhidi ya Taifa Stars.
 
The Scorpions ilipaswa kubadili ndege Dakar, Senegal jana usiku lakini kukawa na ucheleweshaji (delay), hivyo ikashindwa kuwahi Nairobi, Kenya ambapo ingeunganisha kwa ndege ya alfajiri kuja Dar es Salaam.
 
Kikosi cha timu hiyo chenye wachezaji 22 wakiwemo tisa wanaocheza mpira wa kulipwa nje ya nchi hiyo kitafikia kwenye hoteli Sapphire iliyopo Mtaa wa Lindi na Sikukuu eneo la Kariakoo.
 
Wachezaji walioko katika msafara huo ni Musa Camara, Abdou Jammeh, Momodou Futty Danso, Lamin Basmen Samateh, Ousman Koli, Pa Saikou Kujabi, Mustapha Kebba Jarju, Yankuba Mal Ceesay na Demba Savage.
 
Wengine ni Saihou Gassama, Alieu Darboe, Momodou Ceesay, Pa Modou Jagne, Tijan Jaiteh, Bubacarr Sanyang, Christopher Allen, Musa Yaffa, Sulayman Marr, Mamut Saine, Hamsa Barry, Ali Sowe, Omar Colley na Saloum Faal.
 
PROGRAMU YA MAZOEZI YA GAMBIA
 
IJUMAA JUNI 8
01.00 asubuhi Mazoezi- Uwanja wa Karume
10.00 jioni   Mazoezi- Uwanja wa Taifa
 
JUMAMOSI JUNI 9
04.00 asubuhi  Mkutano na Waandishi wa Habari- Ukumbi wa TFF
10.00 jioni  Mazoezi- Uwanja wa Taifa
 
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)


Comments