WASANII KIBAO KUPAMBA SHEREHE ZA CHELSEA BONGO


Katibu wa mashabiki wa Chelsea tawi la Tanzania Clifford Ndimbo (kati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na sherehe za ubingwa hapa nchini zitakazofanyika jumapili katika ukumbi wa msasani Beach, kulia ni msanii Rama na kushoto ni Christian Bella wote kutoka Akudo Impact.

CHELSEA Tanzania leo imewatangaza wasanii watakaopamba sherehe za ubingwa zitakazofanyika kwenye ukumbi wa Msasani Beach Club Jumapili hii.
Mbali na michezo itakayozikutanisha Chelsea Tz,Arsenal Tz na Manchester Tz pia kutakuwa na burudani mbalimbali wakiwemo Mr.Nice,Sweet Sunday,Muumin Mwinyjuma,Charles Baba,Shilole atakayesindikizwa na Irene Uwoya na Akudo Impact.
Kiingilio kitakuwa shilingi elfu 10 kwa wakubwa na watoto shilingi elfu 1.
Sherehe hizo zitaanza tokea saa 4 asubuhi kwa soka la ufukweni.
Sherehe hizo ni mwanzo tu wa mambo mengi makubwa yatakayofuata baada ya usajili wa Taasisi itakayotambulika pia makao makuu huko London.
Cliford Mario Ndimbo
Katibu wa Chelsea Tz