WASANII BONGO MOVIE WATOA MSAADA WA VYANDARUA HOSPITALI YA BOMBO JIJINI TANGA HII LEO

Wasanii wa Bongo Movie wakiongozwa na Mwenyekiti wao Jacob Steven "JB" wakiwa kwenye picha ya pamoja na Muuguzi Msaididi wa Hospitali ya Rufaa ya Bombo jijini Tanga.Wasanii hawa wametembelea Hospitali ya Bombo mapela leo asubuhi kwa ajili ya kukabidhi msaada wa Vyandarua katika hospitali hiyo,ikiwa ni sehemu ya kupiga vita ugonjwa wa Malaria unaopoteza maisha ya watanzania wengi katika maeneo mbali mbali ya nchini.Msaada huo umekabidhiwwa hospitalini hapo kwa hishani ya kampuni ya Bia Tanzania Kupitia kinywaji Chake cha Grand Malt ambao ni wadhamini wakuu wa Tamasha la Filamu za Kitanzania (Bongo Movie) linalozinduliwa leo hii kwenye Viwanja vya Tangamano Jijini Tanga.Picha na Othman Michuzi
 Mwenyekiti wa Wasanii wa Bongo Movie,Jacob Steven "JB" akikabidhi msaada wa vyandarua kwa Muuguzi Msaididi wa Hospitali ya Rufaa ya Bombo jijini Tanga,pia Mwalishi wa Hospitali hiyo,Bi. Halima Msengi (kushoto) wakati wasanii hao walipotembelea hospitali hiyo na kujioneea hali halisi ya uhaba wa vyandarua katika baadhi ya wodi.Msaada huo umekabidhiwwa hospitalini hapo mapema leo asubuhi kwa hishani ya kampuni ya Bia Tanzania Kupitia kinywaji Chake cha Grand Malt ambao ni wadhamini wakuu wa Tamasha la Filamu za Kitanzania (Bongo Movie) linalozinduliwa leo hii kwenye Viwanja vya Tangamano Jijini Tanga.Picha na Othman Michuzi
 Wasanii wa Bongo Movie wakiwa wamezunguka kitanda cha Mmoja wa Mama aliejifungua watoto Mapacha katika Wodi ya Wazazi wa Hospitali ya Bombo Jijini Tanga mapema leo asubuhi wakati walipofika kutoa Msaada wa Vyandarua kwa hisani ya Kampuni ya Bia Tanzania kupitia Kinywaji chake cha Grand Malt ambao ni wadhamini wakuu wa Tamasha la Filamu za Kitanzania (Bongo Movie) linalozinduliwa leo hii kwenye Viwanja vya Tangamano Jijini Tanga.Picha na Othman Michuzi
 Msanii wa Bongo Movie,Mayassa Mrisho akikabidhi Chandarua kwa Mama aliejifungua watoto mapacha kwenye hospitali ya Bombo,Tanga mapema leo asubuhi.Picha na Othman Michuzi.

 Meneja wa Kinywaji cha Grand Malt,Mama Consolata Adam akimjualia hali Mmoja wa kina Mama waliojifungua leo kwenye wodi ya Wazazi,Ndani ya Hospitali ya Rufaa ya Bombo,Jijini Tanga.Picha na Othman Michuzi.

 Wasanii wa Bongo Movie walipoitembelea Wodi ya Wazazi Hospitali ya Bongo,Tanga leo.Picha na Othman Michuzi


Mwenyekiti wa Wasanii wa Bongo Movie,Jacob Steven "JB" pamoja na Katibu wake,Issa Mussa "Claud" wakisaidiana kufunga chandarua kwenye moja ya kitanda cha Hospitali ya Bombo,jijini Tanga mapema leo asubuhi.Picha na Othman Michuzi.