WANACHAMA YANGA SC WAHOFIA KUWASILISHA PINGAMIZI KAMATI YA UCHAGUZI

KAMATI ya uchaguzi ya klabu ya soka ya Yanga mpaka jioni ya leo haijapokea pingamizi lolote juu ya wagombea uongozi katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Julai 15 mwaka huu.
Katibu wa kamati hiyo, Francis Kaswahili (pichani)amesema bado milango ipo wazi kwa mwanachma yoyote anayehitaji kutoa pingamizi na mwisho wa kufanya hivyo ni Juni 18.
Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na blog hii umebaini kwamba baadhi ya wanachama wanahofia kuwasilisha pingamizi kwa baadhi ya waliojitosa kudhamini baada ya kamati ya uchaguzi ya Yanga kutoa tahadhari.
Kamati hiyo inayoongonzwa na Jaji John Mkwawa ilitoa angalizo kwa wanachama wanaotaka kuwasilisha pingamizi kuwa na vielelezi na si kufanya hivyo kwa chuki binafsi na atakayebainika kuweka pingamizi za chuki atalipishwa faini ya sh.500,000 pamoja na kufungiwa miaka miwili.