VODACOM KUWAZAWADIA MABINGWA WA LIGI KUU BARA J'MOSI

                           Simba Sc ndiyo mabingwa wa VPL
                                  AZAM FC (washindi wa pili)
                                   Yanga SC (Washindi wa tatu)

John Bocc wa Azam FC (Mfungaji bora wa VPL)

Kampuni ya Vodacom itakabidhi zawadi kwa washindi wa Ligi Kuu ya Vodacom msimu 2011/2012 katika hafla itakayofanyika Juni 30 mwaka huu kwenye hoteli ya Double Tree Hilton jijini Dar es Salaam. 
Hafla hiyo itakayohudhuriwa na wawakilishi wawili kutoka katika klabu ya Ligi Kuu itaanza saa 12 jioni. Katika hafla hiyo washindi mbalimbali wakiwemo bingwa, makamu bingwa na mshindi wa tatu. 
Wengine watakaozawadiwa ni mfungaji bora, kipa bora, timu bora yenye nidhamu, mchezaji bora wa ligi, refa bora na kocha bora.