TWIGA STARS BAHATI MBAYA TENA FAINALI ZA AFRIKA

 WAchezaji wa Ethiopia wakishangilia
 Kikosi cha kwanza cha Twiga Stars leo
Wanadada wa Ethiopia


MATUMAINI ya timu ya Taifa ya Wanawake 'Twiga Stars' kucheza fainali za Afrika kwa mara ya pili yamepotea leo baada ya kufungwa bao 1-0 na Ethiopia, katika mchezo uliopigwa  kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
 Twiga Stars ilikuwa ikihitaji  walau ushindi wa bao moja tu kujitwalia tiketi ya kwenda kwenye fainali hizo zitakazopigwa  Guinea ya Ikweta, mwezi septemba
Alikuwa ni Berkhatawit Girm aliyeifungia Ethiopia bao hilo katika dakika ya 63 na hivyo kutwaa tiketi ya fainali hizo kwa jumla ya mabao 3-1, baada ya kushinda 2-1 katika mechi ya kwanza.
                                Vikosi vya leo:
Twiga Stars: Fatma Omary, Fatma Khatib, Pulkeria Chalaji, Flora Kayanda, Sophia Mwasikili, Mwapewa Mtumwa, Amina Ally, Eto Mlenzi, Fatma Mustafa, Asha Rashid ‘Mwalala’ na Mwanahamis Omary ‘Gaucho’
Ethiopia: Liya Shibru, Buzhan Endale, Indnshet Tsegaye, Truanche Mengesh, Henot Dengisho, Berkhatawit Girm, Eden Shiferaw, Zulka Juhad, Shetaye Sisay, Birtukan Gebrekirsto na Erehma Zerga.