TENGA AMTETEA YONDANI, ATAKA SIMBA NA YANGA KUYAMALIZA WENYEWE


RAIS wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Leoder Tenga amesema hakubaliana na suala la nyota wa timu hiyo Kelvin Yondan kusaini mikataba miwili na kusema kuwa lazima kuna moja ya klabu imefanya uhuni katika mchakato huo.

Tenga alisema kuwa, kulingana na mfumo wa sasa wa usajili kupitia mtandao, shirikisho lake halihusiki kabisa na usajili na kwamba hilo ni suala la mchezaji na klabu.

“Naamini klabu hizo zitamalizana zenyewe kuhusu mchezaji huyo na akasema suala la Yondan kudaiwa kutoroshwa kambini, Taifa Stars ili akasaini Yanga halina mantiki kwa sababu mchezaji huyo ni mtu mzima ana akili zake timamu, ila kinachoendelea kwa sasa ni kelele za kinazi,”alisema

Wiki iliyopita, beki Yondan aliibuka anasaini Yanga, kabla ya klabu yake, Simba aliyoichezea tangu mwaka 2006 kudai bado ina mkataba naye na wapinzani wao hao wa jadi, wamefanya uhuni kuzungumza naye na kumsajili wakijua hajamaliza mkataba na klabu yake.

Lakini Yondan mwenyewe alikana kusaini Simba na kusistiza amesaini Yanga tu, waliompa Sh. Milioni 30 kwa mkataba wa miaka miwili.