SIMBA SC WAMSHIKA UCHAWI KIGOGO TFF

MABINGWA wa ligi kuu soka Tanzania bara Simba SC wamesikitishwa na kitendo cha Mkurugenzi wa mashindano wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) Saad Kawemba kudai Kelvin Yondani ni mchezaji huru.
Ofisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga alisema jana kwamba wanashangazwa na matamshi ya Kawemba kwa kuwa TFF haifanyi usaijili zaidi ya kuhifadhi mikataba ya wachezaji ili kama kuna tatizo waipitie.
"Suala hilo inabidi lipelekwe kwa kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji  ambao ndio wanauwezo wa kutoa jiubu sahihi lakini kwa kauli ya Kawemba inaonyesha kuna wasioitakia mema Simba Sc,"alisema.
Aliongeza kuwa tayari rais wa TFF Leodger Tenga ameagia uchunguzi ufanyike, lakini inashangaza kiongozi wa TFF kuzungumzia suala hilo wakati hata uchunguzi bado haujakamilika.
Hatua hiyo inafuatia Yondani kuitaliki Simba na kwenda kusajili Yanga kwa dau la Milioni 30,000 huku Simba ikidai bado ina mkataba na mchezaji huyo.