SIMBA SC KUSAKA UBANI WA MAPINDUZI VISIWANI ZANZIBAR

MABINGWA wa  mpira wa Miguu Tanzania Bara Simba Jumatatu wataondoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar kuweka kambi ya  kujiandaa na michuano ya Kagame ikiwa ni kushiriki michuano ya Utafiki inayofanyika visiwani humo.
Makamu Mwenyekiti wa Simba Geofrey Nyange Kaburu' alisema kuwa timu hiyo itaondoka Jumatatu asubuhi 
ikiwa ni baada ya mchezo wao wa Jumapili dhidi ya Express ya Uganda.
Kaburu alisema kocha mkuu wa timu hiyo Milovan Cirkovick, ameomba apate mecho moja kabla ya kwenda visiwani huko ambako watarejea siku moja kabla ya kuanza kwa michuano ya Kagame.
Alisema kuwepo kwao Zanzibar kutasaidia kuipa timu yao mazoezi mazuri kama wanavyofanya kila wakati wanapokuwa na michuano au mechi muhimu.

"Tutakaa Zanzibar kwa muda wa wiki mbili lengo letu ni kikosi chetu kiwe kizuri tyutashiriki michuano na kuweka kambi kama tunavyokaaga"alisema Kaburu.


Wakati huo huo mchezaji Mussa Mode, jana alianza rasmi mazoezi katika kikosi cha timu hiyo ambapo mchezaji huyo aliamsha shangwe kutoka kwa mashabiki lukuki 
waliyoudhurtia mazoezi ya timu hiyo baada ya kuwasili na kuanza  mazoezi.