SIMBA SC HAINA MPANGO NA NSAJIGWA

MABINGWA wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba wamesema hawana mpango wa kumsajili aliyekuwa nahodha wa Yanga, Shadrack Nsajigwa.
Kiongozi mmoja wa Simba ameiambia mamapipiro blog kwamba anashangazwa na taarifa za baadhi ya vyombo vya habari kuwepo na mpango wa kumsajili nyota huyo aliyetupiwa virago Jangwani.
Alisema ni vigumu kwao kumsajili nahodha huyo wa zamani wa timu ya Taifa 'Taifa Stars'kutokana na kiwango chake kushuka sambamba na kuwa na umri mkubwa.
"Tunashangazwa na taarifa hizo kwa kweli, ni vigumu kumsajili Nsajigwa kwani kiwango chake kimeshuka pia umri umesonga...bora wangemuacha mtu kama Niyonzima (Haruna) tungemsajili lakini si Nsajingwa,"alisema.