SIMBA KUWATOA WANNE KWA MKOPO, KAGO, JJ WAMALIZA MKATABA


Mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania Bara Simba wanakusudia kuwatoa kwa mkopo katika vilabu mbalimbali nyota wake wanne wakiwemo Rajab Isihaka, Salum Machaku, Haruna Shamte na Shija Mkina.
Ofisa habari wa Shirikisho la soka Tanzania Boniface Wambura amesema kwamba Simba imewasilisha taarifa hiyo na kuwataja wachezaji waliomaliza mikataba yao ni pamoja na  Ally Mustafa, Derick Walulya, Gervais Kago, Juma Jabu wakati Salum Kanoni mkataba wake unatarajia kumalizika Juni 30 mwaka huu.

Comments