SIMBA KURUDIANA NA EXPRESS J'2 UWANJA WA TAIFA


MABINGWA wa soka wa Tanzania, Simba SC, jumapili wanatarajiwa kucheza na mabingwa wa soka wa Uganda, Express FC, katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliopangwa kuchezwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 
Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Simba, Evodius Mtawala, maandalizi yote kwa ajili ya pambano hilo yamekamilika na kwamba kikosi cha Simba kitaundwa na wachezaji wapya na wa zamani .
Mechi hiyo itakuwa ya marudinao kwa mabingwa hao ambapo mechi ya awali walicheza katika dimba la Kambarage mijinio Shinyanga Jumamosi iliyopita na kutoka sare ya bao 1-1