SHEIKH 'ABRAMOVICH' KUENDESHA HITMA JANGWANI KESHO


 Mzee ibrahim Akilimali 'Abramovich'

KLABU ya soka ya Yanga kesho  inatarajiwa kuendesha kisomo maalum ‘hitma’ kwa ajili ya kuwarehemu wanachama, mashabiki, wapenzi na wachezaji wa timu hiyo waliotangulia mbele ya haki ambapo zoezi hilo litafanyika makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo mitaa ya jangwani na Twiga na kuongozwa nma katibu wa baraza la wazee, Ibrahim Akilimali 'Abramovich'. 
“KAma mnavyojua kila msimu mpya wa ligi kuu soka Tanzania bara unapokaribia kuanza huwa tunasoma dua ya kuwarehemu wadau mbalimbali wa Yanga waliotangulia mbele ya haki hivyo kesho ijumaa majira ya saa sita mchana hapa klabu tutaendesha kisomo hicho ambacho kitaongozwa na Sheikh Akilimali (Ibrahim) hivyo tunaomba wanayanga kujitokeza kwa wingi,”alisema Sendeu. 
Sendeu aliongeza kuwa baada ya dua hiyo jioni ya leo kutakuwa na mkutano maalum utakaohusisha wenyeviti na makatibu wa matawi yote ya Yanga ya jiji la Dar es Salaam.