RASMI:ASAMOAH ATEMWA YANGA SC


WAKATI mchakato wa vilabu vya ligi kuu soka Tanzania Bara kuwasilisha majina ya wachezaji wanaoachwa ama kumaliza mikataba ukifikia tamati keshokutwa, klabu ya Yanga kesho itawasilisha majina hayo kwa shirikisho la soka Tanzania (TFF) ambapo katika orodha ya wachezaji walioachwa yumo nyota wake wa kimataifa Mghana Kenneth Asamoah (pichani). 
Ofisa habari wa Yanga Louis Sendeu amesema leo kwamba  klabu yake imewaacha wachezaji 15 ambapo kati yao kuna waliomaliza mikataba yao na wengine kupelekwa kwa mkopo katika vilabu vingine vya ligi kuu soka Tanzania Bara. 
Aliwataja wachezaji waliachwa mbali na Asamoah ni pamoja na mshambuliaji wa kimataifa Mzambia Davies Mwape, Iddi Mbaga, Julius Mrope, Kiggi Makassi, Atif Amour, Abuu Ubwa, Zuberi Ubwa, Bakari Mbegu, Godfrey Bonny na Shaban Kado ambaye amepelekwa kwa mkopo katika klabu ya Mtibwa Sugar.