POLISI JAMII CUP KUANZA KESHOKUTWA KINONDONIMkuu wa Polisi wilaya ya Kipolisi Kinondoni, Willbroad Mutafungwa,(kulia)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, hawapo pichani juu ya kuanza kwa michuano ya Polisi Jamii katika wilaya hiyo michezo itakayoanza kesho kutwa ikitanguliwa na uzinduzi utakaofanyika kesho katika uwanja wa Polisi Osterbay, kushoto kwa Mutafungwa ni Afisa Polisi jamii tarafa ya Kinondoni, Inspekta msaidizi wa Polisi, Mkweru N. Maswale.


Michuano ya polisi jamii kwa wilaya ya kipolisi Kinondoni, inatarajiawa kuanza keshokutwa huku ikitanguliwa na mchakato mzima wa uzinduzi utakaofanyika kesho katika viwanja vya polisi Osterbay. 
Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kipolisi, Kinondoni Willbroad Mutafungwa alisema michuano hiyo itashirikisha vijana kutoka kata nane zinazounda wilaya ya Kipolisi ya Kinondoni. 
Alizitaja kata hizo kuwa ni Kinondoni ,Msasani,Mikocheni,Mwananyamala,Makumbusho, Hananasif, Kijitonyama na Makongo huku akitaja aiana ya michezo kuwa ni mpira wa miguu, kuvuta kamba na kukimbiza kuku Mutafungwa ambaye pia ni mwenyekiti wa maandalizi ya michezo hiyo ya polisi jamii Cup, alisema kabla ya michezo hiyo kuanza kutakluwa na utoaji wa elimu kwa vijana amabao ni walengwea wakuu wa michuano hiyo. 
“Tunataka tuwafikie vijana zaidi kwa kuwa wao ndiyo waathirika wa matendo mbali mbali ya kihalifu, na kwa kutumia michezo tunataraji wengi watakuwa na shughuli za kufanya na kujiondoa katika matendo ya uhalifu”alisema Mutafungwa. 
Alisema maandalizi kwa kata zote nane zimeshakamilika na kinachosubiriwa ni wakati ufike ili vijana waanze kuonyesha uwezo wao katika michezo.