NSAJIGWA, MWASYKA WAREJESHWA YANGA SC


KLABU ya soka ya Yanga imewarejesha kundini nyota wake ambao awali ilipanga kuwatemba Shadrack Nsajigwa 'Fuso' na Stefano Mwasyika, imefahamika.
Habari zilizopatikana jijini leo zinasema kwamba uongozi umweamua kuwarejesha kundini nyota hao kutokana na uzoefu waluionao katika soka hivyo watasaidia kuleta hamasa katika timu.
"kweli ilikuwa tuwateme lakini tumeona timu ina vijana wengi sana sasa uwepo wao utasaidia kwa namna moja ama nyingine, hivyo wachezaji hawa wataendelea kuweopo Yanga,"alisema.
Aliongeza kuwa uongozi unatarajiwa kuketi chini na kuzungumza na Nsajigwa ili kujua tatizo linalonmkabili kiasi kilichopelekea kupoteza mwelekea katika uchezaji wake.