NIYONZIMA AMLETA MRITHI WA MWAPE YANGA SC

KIUNGO wa kimataifa ya Yanga SC , Mnyarwanda Haruna Niyonzima anatarajiwa kuwasili jioni ya leo sambamba na mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Meddie Kagere, imefahamika.
Kiongozi mmoja wa Yanga anayehusika na usajili ameiambia blogu hii kwamba NiyonZima ataambatana na nyota huyo mpya aliyekuwa anakipiga katika timu ya Polisi Rwanda ambaye ataziba pengo la mshambuliaji aliyetupiwa virago wiki iliyopita, Mzambia Davies Mwape.
Amesema mara baada ya kuwasili nchini utafanyika utaratibu wa kuweza kumsainisha mkataba wa kuichezea timu hiyo katika michuano ya kimataifa pamoja na ligi kuu soka tanzania bara.
Tayari Yanga imeanza mazoezi ya kujiandaa na michuano ya kombe la Kagame itakayoanza julai 14 mwaka huu jijini Dar es Salaam ambapo wao ni mabingwa watetezi.