MWAPE ATIMULIWA YANGA SC, WACHEZAJI WAANZA MAZOEZI LEO


KLABU ya  soka ya Yanga mevunja  mkataba wa mshambuliaji wake  Mzambia Davies Mwape. 
Katibu mkuu wa klabu ya Yanga Mwesiga Selestine amesema leo  kwamba, Mwape ambaye alibakiza miezi sita ya kutumikia mkataba wake amelipwa stahiki zake zote.
 “Tumevunja rasmi mkataba na Mwape ambao ulibakiza miezi sita…tayari tunmeshamwandikia barua yake na kumpa stahiki zake zote,”alisema Mwesiga.
Katika hatua nyingine, kikosi cha Yanga chini ya kocha msaidizi Fred Felix Minziro kimeanza mazoezi leokwenye uwanja wa Kaunda ikiwa ni maadalizi ya michuano ya kombe la Kagame inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi julai 11 jijini Dar es Salaam.
 Kupitia mazoezi hayo wachezaji 10 wameripoti wakiwemo Athuman Iddi ‘Chuji’, Godfrey Taita, Oscar Josua, Rashid Idrissa, Yaw Berko, Kenneth Asamoah na Ibrahim Job, huku Nizar Khalfan na Mwape wakishindwa kufanya kutokana na kuwa na maumivu