MSHINDI MISS KIGAMBONI CITY KUNYAKUA 500,000

Mshindi wa taji la urembo kitongoji cha Kigamboni mwaka huu 'MissKigamboni City 2012' atazawadiwa shilingi 500,000 katika shindano
litakalofanyika kesho  katika ukumbi wa Navy Beach jijini Dar es
Salaam.
Mratibu wa shindano hilo, kutoka kampuni ya K&L Media Solutions, Somoe Ng'itu, alisema jana kuwa maandalizi yote yamekamilika  na warembo
wote wako tayari kwa shinda o hilo.
Mratibu huyo amesema kuwa mshindi wa pili atazawadiwa  shilingi laki
tatu na nusu, mshindi wa tatu shilingi laki tatu na washindi wa nne na
watano wataondoka na kitita cha shilingi laki mbili kila mmoja huku
kifuta jasho kwa warembo wengine saba waliobakia kitakuwa ni shilingi
laki moja na hamsini ambapo jumla ya zawadi zote ni shilingili milioni
mbili na laki tatu.
Mgeni rasmi katika shindano hilo atakuwa ni diwani wa kata ya
Kigamboni, DOTTO MSAWA ambaye  ametoa mchango mkubwa katika
kufanikisha shindano hilo.
Aliongeza kuwa ili kuboresha shindano hilo bendi ya muziki wa dansi ya
FM Academia maarufu Wazee wa Ngwasuma na msanii na mchekeshaji mahiri
hapa nchini, Mpoki watatumbuiza kwenye kinyang'anyiro hicho.
"Tunawaomba wadau wa sanaa ya urembo kufika kushuhudia mrembo wa
Kigamboni atakavyopatikana, ni Kitongoji kilichoko sehemu pekee hapa
nchini na kulikosa kushuhudia itakuwa ni kujinyima burudani wewe
mwenyewe," alisema mratibu huyo.

Aliwataja warembo watakaochuana kuwa ni pamoja na Susanne Jeremiah,
Agness Goodluck, Elizabeth Boniface, Dorothea Kessy, Esther Albert,
Edda Silyvester, Sophia Martin, Doreen Kweka, Khadija Kombo, Linnah
David, Rosemary Peter na Winnie Karaya.
Aliwashukuru wadhamini ambao wamejitokeza kusaidia shindano hilo ambao
ni Redd's, Dodoma Wine, hoteli ya Hope Country, Screen Masters, Global
Publishers, Nobro Collections, Times FM na Clouds FM na Kitwe Traders.
Aliongeza kuwa warembo watakaoshika nafasi tatu za juu kutoka katika
shindano hilo wataungana na wenzao kutoka vitongoji vya Kurasini na
Chang'ombe ili kuwania taji la Kanda ya Temeke baadaye mwaka huu.


Comments