Skip to main content

MPENDWA WETU WILLY EDWARD, KUAGWA JUMATANO

 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts Limited, inayochapisha gazeti la Jambo Leo na jarida la Jambo Brand Tanzania, Juma Pinto (kushoto) na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Benny Kisaka (wa pili kushoto) wakiwa kwenye msiba wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa Jambo Leo, marehemu Willy Edward Ogunde ulioopo nyumbani kwa kaka wa marehemu Mburahati, Dar es Salaam leo asubuhi. Wiily amefariki ghafla leo alfajiri mjini Morogoro alikokuwa akihudhuria semina ya siku moja ya masuala ya Sensa. Kutoka kulia ni ndugu zake marehemu; Dennis Ongiri, Joseph Rabach na Julius Rabach.
 Waandishi wa habari wa gazeti la Jambo Leo na Jarida la Jambo Brand Tanzania wakishiriki kwenye msiba wa aliyekuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo Leo, marehemu Willy Edward. Mwili wa marehemu Willy unasafirishwa mchana huu kutoka Morogoro kwenda kuhifadhiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam. Taratibu za mazishi zinaendelea kuratibiwa kwa ushirikiano wa ndungu na viongozi wa Jambo Concepts, lakini kwa mujibu wa Kaka wa marehemu Rabach ni maaishi yatafanyika nyumbani kwao marehemu, mjini Mugumu Wilaya ya Serengeti, mkoani Mara. Siku ya mazishi itatangazwa baadaye.
 jane wa marehemu Willy Edward, Rehema, akiwa kwenye majonzi
 
Mtoto wa mwisho wa marehemu, Willy Edward, Caren akiwa katika msiba Akina mama waombolezaji wakiwa kwenye msiba
 Mtangazaji wa TBC, Grace Kingarame akimfariji mjane wa marehemu Willy Edward, Rehema.
 Mpiga picha wa TBC, Mary Hondo, akimfariji Rehema. 

 Mtoto wa mwisho wa marehemu Willy Edward, Caren (2), akiwa na babake mkubwa, Dennis Rabach
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Jambo Concepts Limited, inayochapisha gazeti la Jambo Leo na jarida la Jambo Brand Tanzania, Juma Pinto akihojiwa na Grace Kingarame wa TBC katika msiba huo. (PICHA ZOTE NA BLOG YA  KAMANDA WA MATUKIO)

 Mbunge wa Jimbo la Morogoro, Azizi Abood, akiwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya New Habari (2006), Husein Bashe wakisubiri kuuona mwili wa Willy Edward
 Baadhi ya waandishi wa habari akiwemo Mbunge wa Morogoro mjini, Azizi Abood, wakiwa na huzuni walipokuwa wakisubiri kutoa heshima za mwisho katika Hospitali ya Rufaa ya Morogoro, muda mfiupi kabla ya mwili kusafishwa Dar es Salaam.


Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendera (kulia) akisikiliza jambo kutoka kwa kaka mkubwa wa 
marehemu aliyekuwa mhariri mkuu wa gazeti la Jambo Leo, Willy Edward Ogunde, George Ongiri 
Ogunde muda mfupi kabla ya kuanza safari ya kwenda jijini Dar es Salaam kwa maandalizi ya mazishi katika kijiji cha cha Mgumo kilichopo wilaya ya Serengeti mkoani Musoma. wa pili kutoka kulia ni Katibu Tawala wilaya ya Morogoro, Alfred Shao na kaka mkubwa upande wa baba, Isack Ugunde.