MDENMARK ALETWA KUZINOA TIMU ZA VIJANA

KOCHA wa timu za Taifa ya Vijana waliochini ya miaka 17 na 20 kutoka nchini Denmark atawasili nchini wiki ijayo kwa ajili ya kuanza rasmi kazi ya kuzinoa timu hiyo.

Kocha huyo mrithi wa Kim Poulsen aliyepewa jukumu la kuifundisha timu ya Taifa, Taifa Stars, baada ya aliyekuwa Mdemark mwenza Jan Poulsen kumaliza muda wake.

Rais wa Shirikisho la soka Tanzania a (TFF) Leogegar Tenga, alisema kuwa tayari imeshafanya mazungumzo na makocha zaidi ya watatu kutoka nchini humo.

Alisema kuwa timu ya Taifa Stars ipo chini ya kocha kutoka Denmark ndiyo maana wameamua kumtafutakocha mwingine kutoka nchini humo.

Tenga alisema hata kipindi cha kocha wa timu ya Taifa akiwa Mbrazil Marcio Maximo, alikuwa akileta makocha kutoka nchini humo.

"Tumeongea na Kim ametupa majina ya makocha watatu ambao tumeshaangalia na kuona kuna ambaye atakuja nchini kufanya kazi nasi....na hata alivyokuwa Maximo alikuwa akituambia makocha gani wanafaa nasi tuliamua kuwatafuta"alisema Tenga.