MASHUJAA MUSICA YAWAITA WADAU WA BURUDANI KWENYE BONANZA LA J'2 VIWANJA VYA TCC CHANG'OMBE


BENDI ya muziki wa dansi Mashujaa Wanakibega' kesho Jumapili itaanza rasmi bonanza maalum katika viwanja vya TCC Club Chang'ombe Dar es Salaam.
Akizungumza Dar es Salaam jana meneja wa bendi hiyo Martin Sospeter, alisema kuwa kwa kuanzia Jumapili hii ya Julai mosi itakuwa ikifanya maonesho yake uwanjani hapo na kuanzia saa 4 usiku kufanya tena vitu vyake katika ukumbi wa Business Park uliopo Victoria.
Sopeter alisema kuwa bendi hiyo itakuwa na bonanza lake maalum ambalo linajulikana kama (Mashujaa Sunday Soccer Bonanza) itakayokuwa ikifanyika hapo kila Jumapili.
Alisema burudani kutoka kwa bendi hiyo itaanza saa 9.Alasiri na kumalizika saa 3,usiku.
"Tumejipanga kuwapa wakati wa temeke burudani ndiyo maana tumeamua kuleta burudani hiyo kila Jumapili kuanzia saa 9 kamili tutakuwa maonyesho yake kwa zaidi ya masaa saba ili kila mmoja aweze kuridhika na onesho letu na baadae kuamia Business Park kule makumbusho "alisema Sospeter.
Alisema bendi hiyo chini ya Rais Chalz Baba imejipanga kuhakikisha tunatoa burudani mwanzo mwisho na kuridhisha wapenzi wao.