MASHUJAA MUSICA KUWATUNUKU WATAKAOTINGA 'VIWALO' VYA KIZAMANI IJUMAA

Rais wa Mashujaa Musica, Charlz Baba
BENDI ya muziki wa dansi Mashujaa Wanaposoposo' Ijumaa ya Juni 15 wameandaa shindano maalum la mavazi ya kizamani.
Wapenzi wa muziki wakaovaa mavazi ya kizamani watapata zawadi shindano litakalofanyika kwenye ukumbi wa Business Park Dar es Salaam.
Meneja wa bendi hiyo Martin Sospeter, alisema kuwa watu watakaoingia katikan onesho la bendi hiyo  watapata zawadi.
Alisema wamejipanga kuhakikisha wanatoa zawadi nzuri kwa wapenzi watakakuja katika onesho hilo wakiwa na mavazi ya kizamani, ili na vijana watambue kama nguo za zamani zinaheshima na kutambulika.
Sospeter alisema kila atakayeingia akiwa amevaa vazi la kizamani atakuwa amejiingia katika kushindania zawadi hizo ambazo ni simu za mkononi na pesa taslim.
"Tumejipanga kuhakikisha tunarudisha mavazi ya kizamani ili vijana watambue zamani kulikuwa na mavazi yake ambayo tufauti na sasa na yalikuwa kivuti kikubwa kuliko sasa kila mtu anaamua ajivalie kivvyake"alisema Sopeter.
Alisema bendi yao ya Mashujaa katika usiku huo pia itatuamia nafasi hiyo kupiga nyimbo zao mpya ambazo bado hazijarekodiwa.
Sospeter alisema bendi hiyo chini ya Rais wake Charlz Baba ipo vizuri, ikiwa inajiandaa kurekodi nyimbo zake mpya huku tayari ikiwa imeshatoa nyimbo moja iiitwayo Risasi Kidole.

Comments