MASHUJAA MUSICA KUTUMBUIZA KANDA YA ZIWA

BENDI ya muziki wa dansi Mashujaa Wana Kibega mwishoni mwa wiki hii watakuwa katika ziara maalum Kanda ya Ziwa.
Akizungumza Dar es Salaam jana meneja wa bendi hiyo Martin Sospeter, alisema kuwa onesho la kwanza litafanyika siku ya Ijumaa mjini Kahama Mkoani Shinyanga.
Sospeter alisema Jumamosi ya juni 29 Wanakibega watakuwa mjini  Geita na Jumapili ya Juni 3o watakuwa 
Mkoani Mwanza.
Alisema bendi hiyo iliyopo chini ya Charlz Baba siku ya Jumapili itakuwa kwenye ukumbi wa Villa Park uliopo 
Mkoani humo.
Alisema wameandaa shoo kabambe kwa wapenziwa Mikoa hiyo ikiongozwa na Mwanadada Lilian Internert akiwa na wengine wakali ambao wataonesha shoo zao mpya zilizoundwa hivi karibuni.
Sospeter alisema katika maonesho hayo nyimbo zao zote zitapigwa ikiwa pamoja na zilizokuwa hazijaa kusikika kwenye vyombo vya habari.
"Kuna nyimbo mpya ambazo zitaanza kusikika huko huko tunafanya kama kuwatambulisha wapenzi wa kanda 
ya Ziwa waone mamboi mapya ya Mashujaa"alisema Sospeter.
Alisema bendi hiyo itarejea Dar es Salaam siku ya Jumatatu na kuendelea na ratiba yake ya kila wiki huku 
ikiandaa na ziara yake ya mikoa ya Kusini ambayo itafanyika mwezi ujao.