MASHABIKI WA CHELSEA BONGO KUJIPONGEZA JUNI 24KATIBU Mkuu wa mashabiki wa Chelsea nchini Clifford Ndimbo (Katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na sherehe za ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, kushoto kwake ni mhazini Kwame na kulia ni mujumbe wa kamati hiyo, Rwehure Nyaulawa.


Ndimbo alisema sherehe hizo zitafanyika June 24, mwaka huu, kwenye Ukumbi wa Msasani Club uliyopi Kawe jijini Dar es Salaam na kuongeza kuwa wamewaalika pia mashabiki wa Manchester United na Arsenal.


Aliongeza kuwa Chelsea watacheza mechi na Arsenal na Manchester na mshindi atapewa zawadi, lakini pia kutakua na michezo kwa watoto watakaofika na wazazi wao kwa ajili ya sherehe hizo nao wameandaliwa zawadi.

Viingilio katika sherehe hizo kitakuwa ni Sh, 10,000 watoto ni bure, pia kutakuwa na burudabi mbalimbali ambazo zitatangazwa hapo baadae.