MALAWI YAPATA MWAKILISHI WAKE MISS EAST AFRICA 2012


Mrembo atakayeiwakilisha Nchi ya Malawi katika mashindano ya Miss East Africa 2012 ametangazwa rasmi baada ya kuwashinda wenzake 39 waliojitokeza kutaka kuiwakilisha Malawi katika mashindano hayo.
Mrembo huyo ni Miss Elidas Ella Chirwa (22) mwenye urefu wa 1.82m ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo kikuu cha Malawi.
Fainali za mashindano ya Miss East Africa 2012 zitafanjika tarehe 07 September mwaka huu jijini Dar es salaam ambapo zitashirikisha Nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan, Ethiopia, Malawi, Madagascar, Reunion, Comoros, Seychelles, na Mauritius.
Mashindano ya Miss East Africa yanaandaliwa na kumilikiwa na kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es salaam