KLABU TANO ZAWASILISHA TFF MAJINA YA WACHEZAJI WALIOACHWA/KUKATISHWA MIKATABA


SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF) limepokea majina ya wachezaji walioachwa, kukatishwa mikataba/kumalizika  katika klabu tano za Ligi Kuu ya Tanzania kwa ajili ya usajili wa wachezaji msimu wa 2012/2013.
 Ofisa habari wa TFF Boniface Wambura amesema kwamba   klabu hizo ni pamoja na  Polisi Morogoro iliyopanda msimu huu imeacha wachezaji 17 wakati Tanzania Prisons ambayo pia imepata hadhi ya Ligi Msimu huu imeacha wachezaji 11, huku  Azam ikikatisha  mikataba ya wachezaji watatu.
Uhamisho wa wachezaji kwa msimu huu ulianza Juni 15 mwaka huu na utamalizika Julai 30 mwaka huu wakati kipindi cha kuanza wachezaji (kwa wasio wa Ligi Kuu) ni kati ya Juni 15 na 30 mwaka huu.
 Kwa klabu za Ligi Kuu kutangaza wachezaji watakaositishiwa mikataba yao ni kuanzia Juni 15-30 mwaka huu na usajili wa wachezaji unafanyika kuanzia Juni 15 hadi Agosti 10 mwaka huu.

 Aidha Wachezaji 12 wamemaliza mikataba yao katika klabu ya Kagera Sugar.
Wachezaji walioachwa Polisi Morogoro ni Abdul Ibadi, Ally Moshi, Benedict Kitangita, Hassan Kodo, Hussein Lutaweangu, Hussein Sheikh, Juma Maboga, Mafwimbo Lutty, Makungu Slim, Mbaraka Masenga, Method Andrew, Moses Mtitu, Ramadhan Kilumbanga, Ramadhan Toyoyo, Said Kawambwa, Salum Juma na Thobias John. 
Tanzania Prisons imewaacha Adam Mtumwa, Dickson Oswald, Exavery Mapunda, Ismail Selemani, Lwitiko Joseph, Mbega Daffa, Mwamba Mkumbwa, Musa Kidodo, Rajab Ally, Richard Mwakalinga na Sweetbert Ajiro. 
Wachezaji waliomaliza mikataba yao kwa mujibu wa Kagera Sugar ni Cassian Ponera, Hamis Msafiri, Hussein Swedi, Ibrahim Mamba, Martin Muganyizi, Mike Katende, Moses Musome, Msafiri Davo, Said Ahmed, Said Dilunga, Steven Mazanda na Yona Ndabila. 
Azam imewasitishia mikataba wachezaji Tumba Swedi, Mau Bofu na Sino Augustino. 


Comments