KIM POULSEN AAHIDI USHINDI DHIDI YA MSUMBIJI KESHO


Na Mwandishi maalumu, Maputo 
KOCHA Mkuu wa timu ya taifa, Kilimanjaro Taifa Stars, KimPoulsen amesema kikosi chake kina kazi kubwa katika mechi ya kesho dhidi yawenyeji Msumbuji, lakini ushindi ni lazima. 
Katika mechi ya kwanza iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Stars ilitoka sare ya bao 1-1 na Msumbiji ‘Mambas’. 
Mechi ya kesho itachezwa kwenye Uwanja wa taifa wa Zimpeto jijini hapa. 
Akizungumza  jana mjini hapa, Poulesen raia wa Denmark alisema wachezaji wake katika morali ya hali ya juu na wanachotaka ni kushinda mchezo wa kesho. 
“Msumbiji ni timu nzuri, wanacheza kwa kasi na kila kitu nimekifanyia kazi. 
Ninaamini tutafanyaa vizuri kikubwa ni kufuata maelekezo ya kila tunachotakiwa kufanya,” alisema Poulsen. 
Stars ambayo inadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania kupitia bia ya Kilimanjaro Premium Lager, ilitua hapa Ijumaa na kufanya mazoezi juzi na jana ilitarajia kufanya mazoezi ya mwisho kabla ya mechi hiyo ya
kuwania kucheza KOmbe la Maataiafa Afrika lililopangwa kufanyika nchini Afrika Kusini, Januari mwakani. 
Kwa upande wa nahodha wa Stars, Juma Kaseja alisema ana imani kuba na kikosi chake ambacho kitacheza kwa kujituma.
 “Tunaataka ushindi na tumejiandaa vilivyo, tunajua  Sumbiji ni timu nzuri lakini infungika. 
Morali yetu iko juu na kitu muhimu ni ushindi.
Hakika ushindi ndiyo kitu muhimu,” alisema.
 Kwa upande wa washambuliaji, Mbwana Samatta anayekipiga katika klabu ya TP Mazembe alisema wanaiheshimu Msumbiji lakini bado wanachotaka
hiyo kesho ni ushindi. 
“Tunawaheshimu haina maana tunawahofia, tunataka ushindi. Tunajua bila ushindi hatutakuwa katika nafasi nzuri, tutajitahidi kadiri ya uwezo wetu kufanya vizuri,” alisema.

Comments