IDI AZZAN MGENI RASMI SHEREHE ZA WALIOSOMA KINONDONI MUSLIM


Na Mwandishi Wetu

MBUNGE wa Kinondoni, Bw. Idd Azzan atakuwa mgeni rasmi katika sherehe za wanafunzi waliomaliza shule ya Sekondari ya Kinondoni Muslim (Reunion) zitakazofanyika Jumamosi Juni 30.

Mwenyekiti wa Reunion Bi. Mambo Tambaza alisema katika sherehe hizo ambazo zitahudhuriwa na wanafunzi waliowahi kusoma shule hiyo kutoka ianzishwe mwaka 1966, walimu waliowahi kufundisha shule hiyo na wanafunzi wanasoma watahudhuria.

Makamu Mwenyekiti wa Reunion, Bw. Aboubakar Liongo alisema maandalizi ya sherehe hiyo yamekamilika na sherehe hiyo itaanza saa 5 asubuhi kwenye hoteli ya Cine Club iliyopo Kawe, Dar es Salaam.

Alitoa wito kwa wanafunzi waliowahi kusoma shule hiyo kujitokeza ili kufahamiana na kuangalia uwezekano wa kuisaidia shule hiyo.

"Tumetoa taarifa kwa wanafunzi wote kwa njia ya mtandao na ujumbe mfupi wa simu za mkononi, ni matumaini yetu kuwa wengi watahudhuria" alisema Bw. Liongo.

Katika sherehe hizo mkuu wa shule hiyo na wanafunzi wanaosoma wataeleza hali ya kitaaluma katika shule hiyo na msaada wanaohitaji.