FURSA YA WASANII KUJIFUNZA JINSI YA KUANDAA SCRIPT MAKINI KATIKA FILAMU


JAMES GAYO (MRATIBU)
Wadau wa Sanaa wanataalifiwa kuwa Gaba Art Centre wataendesha warsha ya masaa mawili kuhusu Stadi za uandishi wa miswada ya Sinema ( Script writing skills), Siku ya Jumatatu 18,June 2012, saa 4 kamili kwenye jukwaa la sanaa katika ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) 

Baadhi ya mambo yatakayojadiliwa ni;
1. Namna ya kuendeleza wazo hadi sinema ya kusisimua (Idea to a good film)
2. Namna ya kufikia hisia za watazamaji (Reaching Audience emotion)
3. Ujenzi wa Action na Dialogue nzuri.
3. Kutengeneza Wahusika (Characters)
4. Mfumo wa hadithi, Mwanzo, kati na Hitimisho ( Ploting, beginning, middle and end)

Ni fursa nzuri kwa Wasanii kuleta mabadiliko kwenye tasnia ya filamu kwani kumekuwa na changamoto mbalimbali katika tasnia hii  ambazo kwa njia moja au nyingine zimekuwa kikwazo katika kufikia ufanisi unaohitajika

Mbali ya kukualika wewe binafsi, ninakuomba uwaalike wanachama wako wote wanaoweza kunufaika na mafunzo haya.

KARIBUNI SANA

James Gayo (coordinator)
+255270006

Comments