DOGO ASLAY KUZINDUA MATATU KWA MPIGO


MSANII wa muziki wa bongo fleva  Dogo Aslay anatarajiwa kuzindua albamu, filamu pamoja na kitabu vikibatizwa kwa jina la ‘Naenda Kusema’ , uzinduzi utakaofanyika Juni 24 katika ukumbi wa Dar Live, jijini Dar es Salaam.
Meneja wa kundi la TMK Wanaume Family Said Fella amesema leo  kwamba maandalizi kwa ajili ya uzinduzi huo yanakwenda vema ambapo msanii huyo yupo katika mazoezi makali ya kujiandaa.

Alisema msanii huyo amepania kutoa burudani ya aina yake ambayo itamfanya kila atakayehudhuria onyesho hilo kusuuzika na roho yake hivyo amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi.

Alisema katika uzinduzi huo, Dogo Aslay atasindikizwa na wasanii mbalimbali wakiwemo  TMK Wanaume Family, Mkubwa na Wanawe, Ferooz, Mwan Fa na  Ize Man.