BERKO NJE YA DIMBA SIKU TANO


Golikipa namba moja wa mabingwa wa soka wa Afrika Mashariki na Kati wa Young Africans Sports Club (YANGA), Yaw Berko amepewa mapunziko ya siku tano kufuatia kuchanika katika paji la uso wakati wa harakati za kuokoa mpira katika mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika leo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
 
Akizungumza na  www.youngafricans.co.tz  ,Daktari wa timu Juma Sufian amesema mchezaji huyo ameshonwa jumla ya nyuzi tano katika paji lake la uso hivyo atakuwa chini ya uangalizi kwa kipindi cha siku tano kuanzia kesho akiwa katika mapunziko.

Berko aliumia wakati akiwa katika harakati za kuokoa krosi iliyochongwa na golikipa mwenzake na kuweza kujigonga katika mlingoti wa goli na kusababisha kuchanika na kuweza kupata matibabu ya haraka uwanjani hapo.

Hamis Kiiza akipatitwa matibabu na Dr. Sufian Juma baadaya kuumia sehemu ya kidevu
Mchezaji mwingine aliyeumia katika mazoezi hayo siku ya leo ni Hamis Kiiza Diego ambaye aliumia katika eneo la kidevu baada ya kombora lililoachiwa na mshambuliaji mpya Said Bahanuzi kutua karibu na kidevu chake na kusababisha mchezaji huyo kugaagaa hadi alipopatiwa matibabu na kuendelea na mazoezi hayo.

Mchezaji majeruhi ambaye  hakuweza kufanya mazoezi hayo ni Nurdine Bakari aliyeumia mwanzoni mwa wiki hii.