ALI HASSAN MWINYI MGENI RASMI TUZO ZA TASWA


RAIS mstaafu wa awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya ya utoaji tuzo za wanamichezo bora wa mwaka 2011 zinazotolewa na Chama cha waandishi wa habari za michezo Tanzania (TASWA) zitakazofanyika kesho kwenye ukumbi wa Diamond Jubillee jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taswa Juma Pinto alisema  jana kwamba, chama chake kimeualika Mwinyi kutokana na mchango wake mkubwa katika maendeleo ya michezo hapa nchini.
Alisema maandalizi kwa ajili ya hafla hizo zilizodhaminiwa na kampuni ya bia ya Serengeti Breweries, yanaendelea vema ambapo kituo cha televisheni cha ITV kitarusha Live tukio hilo.
Mshindi wa jumla atazawadiwa kitita cha shilingi milioni 12.5 ambapo wanaowania katika mpira wa kikapu kwa upande wa wanawake ni pamoja na Doritha Mbunda, Evodia Kazinja (JKT Queens), Faraja Malaki (Jeshi Stars), huku kwa upande wa wanaume ni Alpha Kisusi, (Vijana), Filbert Mwaipungu, Gilbert Batungi (ABC), wakati Liliam Sylidion na  Doritha Mbunda watachuana katika Netiboli.
Kwa upande wa gofu wanaowania ni Madina Iddi ,Hawa Wanyeche ,Ayne Magombe kwa upande wa wanawake,wakati kwa wanaume ni Frank Roman,Nuru Mollel na Issac Anania kwa upande wa Wabaume, huku gofu ya kulipwa ni Fadhili Saidi Nkya, Yasini Salehe na Hassani Kadio. 
Ahmada Bakar,Amina Daud Simba (kisahani na tufe),Othman Ally Othman (mkuki, kisahani na tufe) wanawania kwa upande wa Olimpki maalum, huku katika Paralimki ni Zaharani Mwenemti, Joseph Nziku, Yohana Mwila kwa upande wa Wanawake, wakati Faudhia Chafumbwe, Siwema Kilyenyi na Janeth Madise watachuana kwa upande wa wanawake.
Katika ngumi za ridhaa mchuano utakuwa kati ya Suleiman Kidunda,Victor Njaiti na Abdalah Kassim,huku kwa upande wa waogeleaji (Wanawake) ni Magdalena Moshi, Gouri Kotecha, na Mariam Foum na kwa wanaume ni Amaar Ghadiyali na  Omary Abdallah.Judo itawaniowa na Mbarouk Seleman Mbarouk, Mohammed Khamis Jumana Azzan Hussein Khamis.
Wavu (Wanawake) itawaniwa na Zuhura Hassan, Theresia  Ojode (JESHI STARS DAR)na Everlyne Albert wa magereza, huku kwa upande wa Wanaume ni Mbwana Ally, ( MZINGA CORPORATION – MOROGORO),Kevin Peter (MAGEREZA – DAR),Farhan Abubakar ( MAFUNZO ZNZ) na katika ngumi za kulipwa ni Benson Mwakyembe,Nasibu Ramadhan,Francis Cheka,Nassib Ramadhan na Fadhil Majia. 
Watakaowani Tenisi kwa upande wa Wanaume ni Waziri Salum, Omary Abdallah,Hassan Kassim, wakati Wanawake ni Rehema Athuman, Mkunde Iddy na Violet Peter.Baiskeli ni Sophia Hussein,Sophia Anderson kwa upande wa Wanawake, huku Richard Laizer naHamisi Hussein watachuna kwa upande wa wanaume. 
Tuzo ya wachezaji wanaocheza nje itawaniwa na Henry Joseph,Mbwana Samatta-Soka, Sophia Mwasikili (Soka), huku ile ya mchezaji bora chipukizi itwaniwa na Theresia Ojode- wavu (Jeshi Stars),Shomari Kapombe (soka) SIMBA na Salum Abubakari-Azam (soka), wakati mchezaji wan je anayecheza Tanzania ni Haruna Niyonzima-Yanga,Kipre Tchetche-Azam,Emmanuel Okwi-Simba (soka). 
Aidha, tuzo ya mwanasoka kwa wanawake itawaniwa na Asha Rashid,Mwanahamisi Omary (Mburahati Queens),Fatuma Mustapha (Sayari),Eto Mlenzi (JKT), wakati kwa upande wa wanaume ni John Bocco,Aggrey Morris-Azam na Juma Kaseja-Simba, huku katika Riadha Wanawake ni pamoja na Zakia Mrisho,Mary Naali na Jaqueline Sakila wakati kwa upande wa Wanaume ni Dickson Marwa na Alphonce Felix. 
Mikono Wanawake ni Abinery Kusencha (JKT Ruvu),Kazad Mtong (Magereza Kiwira) na Faraji Shaibu Khamis (Nyuki Zbar), huku kwa upande wa Wanaume ni Doris Mangara-(Magereza Kiwira),Zakia Seif (Ngome Dar),Mary Kimiti (Magereza Kiwira) na .Kriketi Wanawake itawaniwa na MoniCa Pascal,Asha Daudi na Esther Wallace, huku Wanaume ni Kassimu Nassoro,Benson Mwita na Riziki Kiseto.