WATOTO HAWA WATAMLILIA DAIMA KANUMBA



Hawa ni baadhi ya watoto walioibuliwa na marehemu Steven Charles Kanumba katika tasnia ya filamu ambapo wameonyesha vipaji vyua hali ya juu kupitia filamu kadhaa walizoshirikishwa zikiwemo Uncle JJ, Big Daddy na nyinginezo.
Kusema kweli ni kama mshumaa uliokuwa ukiwaangaza watoto hawa umezimika ghafla hivyo kuwaacha katika kiza kizito cha majonzi watoto hawa ambao ni hazina ya baadaye katika ulimwengu wa sanaa.
Yote kwa yote ni kazi yake mola ambayo haina makosa, kikubwa ni kumuombea kwa mwenyezi mungu marehemu Kanumba apumzike kwa amani, Amina

Comments