MILOVAN AWASOMA AL AHLY KUPITIA VPL

KOCHA mkuu wa Simba Mserbia Milovan Cirkovic amesema mechi tatu za Ligi Kuu soka Tanzania Bara zimemewezesha kubainia mapungufu yaliyopo kwenye kikosi chake.
Milovan amesema kuwa kupitia mechi hizo amebaini mapingufu yaliyopo kwenye kikosi chake hivyo atayafanyia kazi kabla ya mchezo wake wa kombe la Shirikisho (CAF) dhidi ya Al Ahly Shandy ya Sudan utakaochezwa April 29 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo Milovan alisema kikosi chake hakiko vibaya sana zaidi ya kuhitaji marekebisho madogomadogo tu.

Comments