AFANDE SELE AUTAKA UBUNGE


MFALME wa Rhymes nchini Seleman Msindi 'Afande Sele' ameweka wazi mpango wake wa kugombea ubunge katika uchaguzi wa mwaka 2015.
Akizingumza hivi karibuni Sele alisema ameamua kugombea ili kuweza kuwatetea wanyonge ambao wamekosa watetezi bungeni.
Hata hivyo Msindi ambaye amekuwa akiimba nyimbo zenye 'mguso' kwa jamii zikiwemo 'Mtazamo' aliowashirikisha Solothang na Prof.J,Karata Dume na nyinginezo hakuweka wazi kuwa atasimama kwa tiketi ya chama gani.