BINTI WA WHITNEY HOUSTON ATAKA KUJINYONGA

WHITNEY HOUSTON

BOBBI KRISTINA

BAADA ya kutokea kwa kifo cha mwimbaji, Whitney Houston kumeibuka kwa taarifa mbalimbali huku nyingine ambazo zimeendelea kuchukua nafasi ni binti yake  Bobbi Kristina (18), ambaye amekimbizwa hospitalini mara mbili tangu kufariki kwa mama yake.

Kifo cha mwanamama huyo kimeishtua dunia na kuwa gumzo kimehusishwa na kutumia dawa za usingizi kupita kiasi na pombe.

Sababu ya kusema hivyo imeelezwa kwamba amekutwa amefariki ndani ya maji wakati akiwa anaoga kwenye bafu la hoteli ya Beverly Hilton chumba cha kifahari namba 434 aliyokuwa anaishi kabla ya kupatwa na umauti.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo wanasema kwamba wakati alipoingia bafuni kuoga walishangaa amekaa kwa muda mrefu na ndipo walipoanza kugonga lakini bila majibu, ikambidi mtengenezaji wake wa nywele afungue mlango na kumkuta akiwa amelala kifudifudi juu ya maji.

Ndipo alimuita mlinzi wa mwanamama huyo akaingia na kumvuta ambako walimpeleka hospitali wakamchukulia vipimo na kugundua tayari alikuwa ameshafariki.

Kuna taarifa nyingine zinazosema kwamba siku moja kabla ya kifo alionekana akiwa kwenye baa ya hoteli hiyo akinywa kinywaji huku wengine wakimuhusisha na matumizi ya dawa za kulevya.

Kifo cha mwanamama huyo kimesababisha binti yake mwenye miaka 18, Bobbi Kristina kuchungwa kwa makini akihofiwa huenda anaweza kuchukua uamuzi wa kujingonga.

Houston (48) kabla ya kifo chake amekuwa akisemwa kujihusisha na matumizi ya dawa za kulevya ambako inadaiwa inawezekana atakuwa ametumia dawa hizo wakati akiwa amelewa.

Baada ya msako chumbani mwake zilikutwa chupa za Lorazepam, Valium, Xanax na dawa nyingine za usingizi ambazo wakati mwingine hutumiwa na mateja kama kilevi halim inayowasababisha wengi kuamini kwamba inawezekana baada ya kunywa pombe alichukua dawa hizo na kutumia.

Pamoja na maneno hayo yote ofisa wa Los Angeles alikana taarifa zilizokuwa zikimuhusisha mwanamama huyo na kufariki kutokana na maji aliyokuwa akioga kudaiwa kuingia kwenye mapafu yake.

Alisema kwamba taarifa zote zimebaki kuwa fununu ila ukweli kamili utaelezwa hapo baadaye baada ya polisi kumaliza upelelezi wake, ambao utachukua zaidi ya mwezi mmoja au miwili hivi, na mpaka sasa bado upo chini ya uchunguzi wa polisi na hakuna anayeruhusiwa kuutembelea na kuutazama mpaka pale watakapowaruhusu kuuondoa.

Baada ya kutangazwa kwa kifo chake aliyekuwa mumewe, Bobby Brown (43) ameripotiwa kuchanganyikiwa na kujikuta akitokwa machozi muda wote baada ya kupokea taarifa za kifo hicho alijikuta akiwaliza mashabiki waliokuwa wamehudhulia onesho lake la huko Mississippi, Marekani, alilokuwa akipiga na bendi yake ya New Edition ambako alisikika akilia kwa sauti akisema “nakupenda Whitney” huku akipiga busu hewani.

Baada ya kifo chake kilichotokea muda mchache kabla ya kufanyika kwa tuzo za Grammy mwimbaji Jennifer Hudson aliimba nyimbo ya heshima kwa ajili ya gwiji huyo wa muziki.

Naye rafiki wake wa karibu na mwimbaji huyo Mariah Carey aliongoza kutoa rambirambi kwa kusema “Nimevunjika moyo na machozi yananitoka kwa kifo cha rafiki yangu mpenzi Whitney Houston, hatatokea mwanamuziki mwingine mwenye sauti nzuri kama yake duniani."

Naye mwimbaji Christina Aguilera aliandika kwenye Twitter akisema “Tumepoteza gwiji mwingine. Tuwaombee familia ya Whitney kwa kumpoteza mtu muhimu."

Gwiji wa miondoko wa Aretha Franklin, alisema ameshtushwa na habari hizo na kuongeza “Siwezi kusema lolote kwa sasa ila bado siamini nilichokisikia. Sikuamini maneno yaliyokuwa yakipita kwenye kioo cha TV yangu niliposoma na moyo wangu ukaanza kuwaonea huruma Cissy, binti yake Bobbi Kris, familia yake na Bobby."

Kuna taarifa zinasema kuwa mwaka 2001 baada ya kifo cha mfalme wa Pop kuliibuka uzushi uliokuwa ukimuhusisha na kufariki siku ya pili.

Mahusiano

Mwaka 1980 mwimbaji huyo akiwa maarufu alianza kujihusisha katika mahusiano na mchezaji wa soka ya Marekani, Randall Cunningham na mwigizaji Eddie Murphy. Mwaka 1989 alikutana na mwimbaji wa R&B, Bobby Brown katika sherehe za utoaji wa tuzo za Soul Train Music na hapo walianza mahusiano rasmi yaliyodumu kwa miaka mitatu na Julai 18, 1992 kutangaza ndoa.

Machi 4, 1993 wawili hao walipata binti yao wa kwanza, Bobbi Kristina Houston Brown.

Mahusiano ya wawili hao yalikuwa katika wakati mgumu baada ya kubanwa na kashfa za kutumia dawa za kulevya kwa kila chombo cha habari.

Pamoja na mara kadhaa kugoma kukubali hilo ila mwaka 2009, Whitney alikiri kwenye kipindi cha TV cha Oprah Winfrey alikiri na kusema kwamba walianza kwa na mumewe wa zamani Bobby Brown, kuvuta bangi na baadaye kokeini.

Katika kipindi hicho alibainisha kwamba sababu kubwa ya kutumia dawa za kulevya ilichangiwa na kutaka kumfurahisi mumewe huyo aliyekuwa akimpenda ambaye alikuwa amethirika na dawa hizo za kulevya.

Akasema “kuna wakati ulifikika dawa za kulevya zilikuwa ndio kila kitu katika maisha yake, na nisipotumia sipati furaha na nilipotumia kuna wakati nilijikuta napoteza njia."

Oktoba 1994, Houston alipiga muziki katika sherehe ya chakula cha usiku katika Ikulu ya Afrika Kusini wakiwa wamearikwa na rais wa nchi hiyo, Nelson Mandela ambaye alimpigia debe na kumuwezesha kushinda uchaguzi wa kwanza wa kuondoka kwa ubaguzi wa rangi.

Mwigizaji huyo baada ya kupata matatizo hayo yaliyoonekana kuchangiwa zaidi na dawa za kulevya alichukua uamuzi wa kutengana na Boby mwaka 2007 aliyemuona kama mtu aliyechangia kuharibu maisha yake kwa kumsababishia kuwa teja na pia alimlaumu kwa kumpatia kipigo kila wakati.

Muda mfupi baada ya kutangaza kutengana na Boby aliripotiwa kuwa katika mahusiano ya kimapenzi na mdogo wa mwaimbaji, Brandy anayekwenda kwa jina la Ray-J ambaye kwa wakati huo alikuwa na umri wa miaka 17 hiyo ilikuwa mwaka 2007 na 2009.

Jambo hilo lilisemwa kila kona hali iliyosababisha hata Bobby Brown, kumtishia kijana huyo akifikiria sababu kubwa ya kutengana na mkewe huyo ilichangiwa na mahusiano hayo.

Unapozungumzia mwaka 1980 hadi 1990 mwimbaji huyo alikuwa mwimbaji anayeongoza kimauzo, mwenye sauti ya mvuto na yenye nguvuna mwigizaji aliyetamba na filamu kama vile ‘The Bodyguard’ na ‘Waiting to Exhale.’

Uwezo wake wa kuimba ulichangia kwa kiasi kikubwa kuibua vipaji vya waimbaji ambao nao wamekuwa moto kama vile Christina Aguilera, Mariah Carey.