PAPIC AWATIMUA KIIZA, MBUNA


WAKATI kocha wa Yanga, Mserbia Kostadin Papic akipendekezwa kuvunjwa kwa mkataba wa beki wa kimataifa wa timu hiyo Hamis Kiiza, uongozi umeazimia kumtimua Beki wakeFred Mbuna.
Maazimio hayo yalifikiwa katika mkutano baina ya benchi lka ufundi, kamati ya mashindano na ile ya usajili ya klabu hiyo kwa ajili ya kujadili mustakabali mzima wa wachezaji watakaoitumikia timu hiyo katika mzunguko wa pili wa ligi kuu bara na michunao ya kimataifa.
Habari zinaeleza kwamba, Papic amedai kutoridhishwa na kiwango alichokionyesha Kiiza kama mchezaji wa kimataifa, hivyo kama inawezekana mkataba wake uliobakiza miezi sita uvunjwe na kulipwa stahiki zake.
Aidha, imedaiwa Mbuna hana budi kuachwa kundini kutokana na umri wake kuwa mkubwa zaidi hivyo kushindwa kutimiza wajibu wake ipasavyo.

Comments