JUMA PONDAMALI 'MENSSAH' AJIVUA GAMBA

SIKU chache kabla ya kuanza kwa ligi kuu bara msimu wa 2011/2012 kocha wa timu ya Villa Squad Juma Pondamali 'Menssah' amejiuzulu kuifundisha timu hiyo.
Menssah amefikia maamuzi hayo kwa madai kwamba moja ya sababu iliyomfanya aachane na timu hiyo aliyoiwezesha kupanda daraja ni matatizo katika ulipwaji wa posho zake toka kwa viongozi wa timu hiyo.
Alisema baada ya kuachana na timu hiyo sasa atakuwa akiinoa timu ya Magomeni City ambayo inashiriki Ligi ya TFF ngazi ya Wilaya ya Kinondoni .

Comments