ALI CHOKI APUNGUZA WASANII TWANGA PEPETA

ALI CHOKI MWENYE TISHETI YA MISTARI AKIWA NA BAADHI YA WASANII ALIOWANYAKUA TOKA TWANGA PEPETA.(Picha kwa hisani ya www.fullshangwe.blogspot.com).

BENDI ya muziki wa dansi ya Extra Bongo jana ilitangaza kuwachukua wanamuziki wanane kutoka The African Stars ‘Twanga Pepeta’.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika ukumbi wa Rufita Sinza jijini Dar es Salaam, jana, Mkurugenzi wa Extra Bongo, Kamarade Ally Choki aliwataja nyota hao walionyakuliwa kutoka Twanga kuwa ni pamoja na Roggert Hegga ‘Caterpillar’, Rapa Saulo John ‘Ferguson’, wapiga magitaa Hosea Simon na God Kanuti aliyekuwa mkali wa Solo.
Wengine ni wanenguaji Mussa Hassan ‘Nyamwela’ na Otilia Boniphace.

Comments