MIRIAM GERALD KUVUA TAJI LA PILI AGOSTI 7


MISS TANZANIA, Miriam Gerald natarajiwa kuvua taji lake la pili kupitia shindano la Miss Kanda ya Ziwa kwa mwaka 2010 linalotarajiwa kufanyika Agosti 7 katika hoteli ya Natiro Annex jijini Mwanza ambapo warembo 24 watachuana.



Mratibu wa shindano hilo lililoandaliwa na Clara Salon & Boutique Winston Mwasambili alisema jana kwamba warembo watakaochuana wanatoka katika mikoa ya Kagera, Shinyanga, Mara na wenyeji Mwanza.

Aliwataja warembo hao kuwa ni Fatuma Ibrahim, Jacquiline Sospeter, Halima Ismail (Mara), Mtuli Ibrahim, Magreth Godson, Hadija Amir (Shinyanga)Agatha Malembeka, Suzan Kessy na LIliaan,  Rosemary Chedima, Fide Deogratius, Leah Patrick, Anastazia Deogratius na Happines Israel kutoka Mwanza.

Comments