RBP MISS DAR INTERCOLLEGE KUWASHANGILIA TWIGA STARS KESHO












Baadhi ya washiriki wa RBP Miss Dar Intercollege wakimsikiliza mwalimu wao Beatrice Lukindo

Baadhi ya wachezaji wa Twiga Stars wakiwa mazoezini





WAREMBO watakaoshiriki shindano la RBP Miss Dar Inter college 2010 kesho wanatarajiwa kuipa nguvu timu ya taifa ya wanawake ‘Twiga Stars’ katika mechi yao dhidi ya Eritrea itakayopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.


Mratibu wa shindano hilo, Silas Michael, warembo hao watahudhuria mechi hiyo kwa ajili ya kuwashangilia, ili kuwapa moyo Twiga Stars waweze kucheza kwa nguvu zote na hatimaye kuibuka na ushindi.

Alisema, mahudhurio hayo ni sehemu pia ya mikakati ya mlezi wa timu hiyo, Rahma Al Kharoos ambaye amedhamini shindano hilo, aliyepanga kuipeleka Twiga Stars nchini Marekani Juni mwaka huu kwa ajili ya kujinoa zaidi endapo itafanikiwa kuiondosha Eritrea.

Shindano la RBP Miss Dar Intercollege linatarajiwa kufanyika Mei 27 kwenye ukumbi wa Club Bilicanas, ambako warembo 15 watapanda jukwaani kuwania taji hilo wakisindikizwa na wasanii wa bongo fleva Amin na Barnabas.

Shindano limedhaminiwa na  RBP Oil Industrial Technology Tz Limited, Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia kinywaji cha Redd’s Original, Tanzania Daima, Vodacom Tanzania, Shear Illussion, Condy Bureau De Change, Ndege Insurance, Dotnata Decorations na Club Bilicanas.

Comments